Hivi karibuni kumekuwa na mfululizo wa ongezeko la misiba. Natambua si kila msiba unasababishwa moja kwa moja na ugonjwa unatokana na virusi vya corona (COVID-19) lakini ni ukweli pia kwamba kuna ambayo inasababishwa kwa virusi hivyo.

Kijamii, nyakati hizi si nyepesi kwani zinaambatana na simanzi na huzuni bila kusahau uwezekano wa ongezeko la wagonjwa wa sonona.

Picha shukrani kwa; Masoud Ally “Kipanya”

Upande mwingine kuna mabadiliko makubwa katika jamii ambayo yanaweza kutokea kwani kwa tafakari pana janga hili lina madhara wakati huu na baada ya kipindi hiki (during and post corona effect). …


Our dream to develop like the European countries still lingers. Under the current regime ‘‘tutakuwa kama ulaya’’ (we will develop like Europe) is the message that has been literally, so invariably, forced into our ears. However, It remains a mere obsession because we are fond of these countries development outcome and don’t give a damn about how they got to where they are.

More specifically, we are not craving for under gird behind the success we see in these countries today. For example, do we know that the foundational stones for their development were built in governance system that delivers…


Nani hajipendi? Nani hajitakii mema? Nani anataka kuchuma janga? Hata wa kwao wana ubavu? Kila kona, kila pahala kauli zachungwa. Mwenendo watazamwa. Kumebaki kupumua, ingawa nako kwa hatua.

Si wenye viti vyao na magari yenye kupumua hadi kwa mkesha hoi maana si mlalahoi tena; atalalaje na hofu tamalaki. Kwani tushasahau yule bwana waliyemtia risasi kule nchi ya ahadi akiwa kimbelembele kutetea haki naam, si haki tu bali haki za weusi wakamshona kwa risasi. Akenda na kuchwa kuhakikisha ajaza jasiri mioyo ya watu kusema mweusi nae mtu. Akiitafuta hata nafsi yake akajiita X; alinena mweusi halali njozi bali anakuwa na usingizi…


Wakati ukuta, kila zama na majira yake. Miaka ikija ikenda. Usiku hufichuliwa na pambazuko. Je, kumeshapambazuka? Tumepambazuka nasi? Nyoyo zetu zi tayari? Je, tunataka mapya au bora liende?

Juni 16, tumeshuhudia safari ya miaka mitano (5) toka 2015 mpaka leo hii 2020 ikiingia tamati kwa wale wenye kuketi kwenye viti vyekundu kwa niaba yetu. Ukomo wa Bunge la 11.

Shukrani/Katuni na; Ali Masoud almaarufu Masoud Kipanya

Mkubwa alifika na kusema yake. Tulimsikia. Kuelewa ni mengine. Kuguswa ni khabari nyingine kabisaaaa…na zaidi kuyeishi hasa na kuona uhalisia napo ni suala jengine. Herufi haziko kuidurusu akisemacho….lah hasha! Hata wale ambao waliona inasomwa na bado mishipa ikashupaa kusema ni bongo…


Kila jambo duniani endapo ukalifanya kwa ufanisi, weledi na ufundi wa hali ya juu hakika utapata utambulisho katika ufanyalo.

Kwa Zanzibar, wapo ambao walikuwa utambulisho na nembo iliyoenda sambamba na kisiwa hicho cha marashi ya karafuu. Bibi Kidude nguli aliyedumu miaka na miaka na kupeperusha bendera vyema ya Zanzibari ni moja tu ya mifano hai.

Hapo ndipo utasikia mtu akijitambulisha natokea Zanzibar; haraka haraka mtu kurukia...oooh kwa Bi. Kidude mwimbaji maarufu...au fukwe nzuri.

Basi bila shaka, jina la Babu Issa nalo limejijengea mizizi na kuwa utambulisho. Yeye upekee wake ni ktk kutengeneza ubuyu wenye ladha ya kipekee. Ndiyo, ubuyu!

Kwa…


Among the questions I do often get are; where are you getting your books? Is this easily available to our bookstores? But also, that experience of thinking on how easily I can get a book or who is coming from abroad that I can direct the books to be dropped in his/her address is a bit annoying especially in these moments with so many changes that have happened and are continue to revolutionize the world.

Bookstores in Dar (which is the busiest, modernized, advanced and populated city within Tanzania) are still countable with few interesting titles to book lovers. …


Adhimisho la Misa Takatifu na Huruma ya Mungu

Sakramenti ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristu ni sakramenti kuu kuliko sakramenti zote kwani ndipo alimo Yesu Kristu mwenyewe mzima; Mwili wake, Damu yake, Umungu wake katika maumbo ya mkate na divai.

Sakramenti hii imewekwa na Kristu mwenyewe wakati wa karamu ya mwisho (Luka 22 :14–20). Kwa njia ya makuhani, Sakramenti hii hufanyika katika adhimisho la Misa takatifu. Tufahamu kuwa, bila Misa hakuna Ekaristi Takatifu na bila Padre hakuna Misa kwani hiyo itaishia kuwa ibada tu. …


Vitabu vilivyonijenga mwaka 2018!

Tunapoelekea kuumaliza mwaka huu, 2018 kama ilivyo ada napenda kuwashirikisha vitabu ambavyo nimemudu kuvisoma.

Naamini kwa kufanya hivi-itakuwa sehemu ya chachu ktk kuamsha na kuimarisha ari ya usomaji vitabu na si vinginevyo mintarafu kujikoga au kuringishia.

Kwa mwaka 2018 nimesoma kikamilifu jumla ya vitabu 18 kulinganisha ilivyokuwa kwa mwaka jana, 2017 ambapo nilisoma vitabu 17.

Orodha hii haitaweka vitabu ambavyo nilianza kuvisoma na kuishia katikati ya njia.

Katika kundi la Falsafa nimesoma vitabu viwili;

  1. Power-Bertrand Russell [Russell ni moja ya waandishi wa Falsafa ambao napenda sana maandiko yake]

2. The Emperor’s Handbook: Marcus Aurelius-C. Scot Hicks…


Taifa la watawaliwa kuliko raia; rahisi kuangamia!

Taifa lolote ili listawi, lina mengi hasa namna gani linawekeza katika watu wake kwa kuwapa elimu bora, kuhakikisha afya zao zinakuwa imara, ili waweze kutumia vyema rasimali kama ardhi na bahari, ziwa na mito katika kujineemesha na kuistawisha nchi.

Kuna umuhimu mkubwa katika yote kuaangalia namna gani rasilimali watu inajengwa na kuimarishwa kama mtaji mkuu wa kwanza wa uhai wa taifa. …


Corpus Christi; Mwili na Damu Takatifu ya Yesu Kristu!

Kanisa kwa namna ya pekee limetenga siku ya kuadhimisha mwili na damu takatifu ya Yesu Kristu ama kwa kilatini Corpus Christi baada tu ya adhimisho la Utatu Mtakatifu. Kwa kutumia siku hii; tunapata fursa kutafakari, kumkiri na kumtangaza Yesu Kristu ndani ya Kanisa na kwa jamii nzima inayotuzunguka. Ni kwa siku hii; Kristu anatembezwa katika jamii yetu kwenye mitaa, njia na kila kona kote duniani kwa shangwe kuu na furaha mithili ya wana wa Israeli walivyotembea na Sanduku la Agano (Rejea: 2 Sam: 12–21).

Kama Sanduku la Agano lilivyokuwa alama na…

Michael Dalali

"Truth is an inseparable companion of justice and mercy"-@pontifex| Cogito Ergo Sum| Analyst| Strategist| Facilitator| Translator| Writer & Avid Reader! 🥋

Get the Medium app

A button that says 'Download on the App Store', and if clicked it will lead you to the iOS App store
A button that says 'Get it on, Google Play', and if clicked it will lead you to the Google Play store